Soma Biblia Kila Siku Mei 2021Mfano
Huwatoa pepo kwa mkuu wa pepo (m.22). Ndivyo walivyodai waandishi waliotoka Yerusalemu, makao makuu ya dini ya Kiyahudi. Waandishi walikuwa ni wanatheolojia na wanasheria wa jamii ya Kiyahudi. Msimamo wao ulikuwa katika mapokeo ya wazee. Mapokeo haya Yesu aliyakataa kuwa si mafafanuzi sahihi ya torati (sheria ya Musa). Kwa hiyo waandishi walidai kuwa Yesu ni mwongo anayemkufuru Mungu, maana alijidai kuwa na amri ya kimungu (ling. 2:5-7, Akamwambia yule mwenye kupooza, Mwanangu, umesamehewa dhambi zako. Na baadhi ya waandishi walikuwako huko, wameketi, wakifikiri mioyoni mwao, Mbona huyu anasema hivi? Anakufuru. Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa mmoja, ndiye Mungu?). Ila Yesu aliwaonya kuwa wakizidi kuifanya migumu mioyo yao watamkufuru Roho Mtakatifu (m.28-30, Amin, nawaambia, Dhambi zote watasamehewa wanadamu, na kufuru zao watakazokufuru zote; bali mtu atakayemkufuru Roho Mtakatifu hana msamaha hata milele; ila atakuwa ana dhambi ya milele, kwa vile walivyosema, Ana pepo mchafu).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Mei 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ayubu. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz