Soma Biblia Kila Siku Mei 2021Mfano
Ujumbe huu ni habari njema kwetu! Tunaona wazi kwamba mbele ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, nguvu za Shetani hazina uwezo wala nafasi. Yesu ni mkubwa, Shetani ni mdogo. Shetani na mapepo yake lazima watii mamlaka ya Yesu! Kwa nini Yesu aliruhusu wenyeji wa pale wapewe hasara ya nguruwe 2000? Maana m.13 inasema, Akawapa ruhusa wale pepo wachafu, wakatoka, wakaingia katika wale nguruwe; nalo kundi lote likatelemka kwa kasi gengeni, wakaingia baharini, wapata elfu mbili; wakafa baharini. Hatujui sababu ya Yesu kutoa ruhusa, lakini huenda aliona kwamba kutokana na tukio hili la pekee habari ya mwujiza wake haitaweza kusahaulika, bali itaenezwa kwa nguvu katika Dekapoli, eneo la kimataifa. Maana tunalojua kwa uhakika ni kwamba Yesu alipokuwa akipanda chomboni, yule aliyekuwa na pepo akamsihi kwamba awe pamoja naye; lakini hakumruhusu, bali alimwambia, Enenda zako nyumbani kwako, kwa watu wa kwenu, kawahubiri ni mambo gani makuu aliyokutendea Bwana, na jinsi alivyokurehemu. Akaenda zake, akaanza kuhubiri katika Dekapoli, ni mambo gani makuu Yesu aliyomtendea; watu wote wakastaajabu (m.18-20).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Mei 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ayubu. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz