Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021Mfano

Elihu anazidi kumsihi Ayubu kwa maelezo kuwa anapaswa kumsikiliza. Anataja malaika, kiumbe kinachotumiwa na Mungu katika kupeleka ujumbe kwa mtu. Ujumbe huo sio bila huruma. Ni kweli, mtu ni mdhambi, lakini Mungu analeta ukombozi. Hakuna ubishi katika hilo. Ila tukumbuke kwamba mwokozi ni Mungu. Mtu hajiokoi na haokoi wenzake. Hivyo, Elihu hawezi kumpatia Ayubu haki. Kazi na sifa hiyo ni ya Kristo tu. Watu waelekezwe katika kusikia wito wa kumjua Mungu na siyo watu wenzao.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Wakorintho na Ayubu. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi tembelea: http://www.somabiblia.or.tz