Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021Mfano
Wale wazee watatu walibainisha kosa la Ayubu na kudai atubu. Elihu anatafuta kumvuta Ayubu kukubali kwamba hajamtambua Mungu sawasawa. Basi, badala ya Ayubu kuendelea kudai Mungu amjibu kama apendavyo yeye, amwombe Mungu kumfundisha ukweli, akitumia ombi katika m.31-32 lisemalo: Mimi nimevumilia kurudiwa, ingawa sikukosa; Nisiyoyaona nifundishe wewe; Kama nimefanya uovu sitafanya tena. Chaguo ni lake Ayubu. Yakupasa wewe kuchagua, si mimi, Elihu anamwambia Ayubu katika m.33. Lakini Ayubu hasemi neno. Kwa hiyo Elihu anajumlisha kuwa Ayubu hana maarifa wala hekima. Ila ikiwa atajaribiwa zaidi, Ayubu angefikia kukubali kurudiwa na Mungu asijibu kama watu waovu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Wakorintho na Ayubu. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi tembelea: http://www.somabiblia.or.tz