Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021

SIKU 19 YA 30

Mtu halingani na Mungu. Mungu ana sifa au majina mawili: Ndiye Mwenye haki na Mtawala. Anayo mamlaka dhidi ya kila mtu na taifa. Wote ni kazi ya mikono yake (m.19). Huu ndio ufahamu wa Elihu. Ayubu amewahi kusema Mungu anamwangalia ili kutafuta sababu ya kumshtaki. Kwa mfano katika 7:17-20 anasema, Je! Mtu ni kitu gani, hata ukamtukuza, Na kumtia moyoni mwako, Na kumwangalia kila asubuhi, Na kumjaribu kila dakika? Je! Hata lini hukomi kuniangalia; Wala kunisumbua hata nimeze mate? Kwamba nimefanya dhambi, nikufanyieje Ee mlinda wanadamu? Mbona umeniweka niwe shabaha yako, Hata nimekuwa mzigo kwa nafsi yangu? Na katika 10:13-14 kuna maneno yanayofanana: Mambo haya uliyaficha moyoni mwako; Najua kuwa haya yamo nafsini mwako; Nikifanya dhambi, ndipo waniangalia, Wala hutaniachilia na uovu wangu. Elihu anajaribu kumsaidia Ayubu kuelewa kwamba Mungu akiwa macho, maana yake ni tofauti na Ayubu anafikiri. Inampa Mungu kuiona miendo yote ya binadamu na hivyo kumwezesha kutawala mambo yote duniani kwa haki.

siku 18siku 20

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021

Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Wakorintho na Ayubu. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi tembelea: http://www.somabiblia.or.tz