Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021

SIKU 21 YA 30

Kuna Wakristo wengi wanaoona kwamba kama wakiacha dhambi, basi ni lazima wapate faida. Ni haki yao. Tena ni haki yao kutoteswa kama Ayubu. Katika somo la leo Elihu anatilia mashaka madai haya. Mbingu zauhubiri ukuu wa Mungu. Basi tujifunze kwamba tutende dhambi, tusitende, haki ina Mungu. Kizuiacho tusione hivyo ni kiburi, na hicho ni ubatili. Hapana asemaye, Yuko wapi Mungu Muumba wangu, Awapaye nyimbo wakati wa usiku; Atufundishaye zaidi ya hayawani wa nchi, Na kutufanya wenye hekima kuliko ndege za angani? Maneno haya ya Elihu katika m.10-11 yanatupeleka kwa Yesu. Tukumbuke asemayo katika Mt 6:33, akituambia kutafuta haki ya Mungu badala ya kutetea na kudai ya kwetu: Utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.

siku 20siku 22

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021

Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Wakorintho na Ayubu. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi tembelea: http://www.somabiblia.or.tz