Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na MatendoMfano

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

SIKU 6 YA 40

Yesu anawateua wanaume kumi na wawili miongoni mwa wanafunzi wake wote kuwa viongozi. Nambari kumi na mbili sio namba aliyochagua kwa bahati mbaya. Yesu anawachagua wanaume kumi na wawili kimakusudi kuonyesha kuwa anakomboa makabila kumi na mawili ya Israeli kwa kuunda kabila mpya. Ila kwa mtazamo wa mwanzo, Israeli hii mpya haionekani kuwa bora kuliko ile ya awali. Yesu anawachagua watu wengi mbalimbali, wasomi na wasio na elimu, matajiri na maskini. Yesu hata anamchagua mtoza ushuru wa zamani aliyefanyia kazi utawala wa Warumi na pia anamteua mwasi wa zamani (mlokole) aliyepigana dhidi ya utawala wa Warumi! Upendo wa Mungu kwa maskini na wageni huwaleta pamoja watu wasiopatana. Inaonekana kana kwamba kamwe hawatapatana, lakini maadui hawa wakubwa wanaacha shughuli zao zote na kumfuata Yesu na kuingia katika utaratibu mpya wa ulimwengu ambapo wanapatanishwa na kuishi kwa umoja.

Luka anatuonyesha kilichoko kwenye utaratibu mpya wa ulimwengu katika simulizi yake ya mafundisho ya Yesu kuhusu Ufalme wa kipekee. Katika mafundisho yake, Yesu anasema kuwa maskini wamebarikiwa kwa sababu wana Ufalme wa Mungu, na kwamba wale wanaolia sasa watafurahi siku moja. Katika utaratibu mpya wa ulimwengu, wafuasi wanapaswa kuwapenda adui zao, kuwa wakarimu kwa watu wasiowapenda, kuwa wenye fadhili na kusamehe. Yesu hakuzungumzia tu kuhusu njia hii ya kuishi. Alionyesha mfano na akawapenda adui zake kwa kutoa dhabihu iliyo kuu zaidi–– kutoa maisha yake.

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo huwahimiza watu, vikundi vidogo, na familia kusoma vitabu vya Luka na Matendo ya Mitume kwa siku 40. Mpango huu unajumuisha video zilizohuishwa na mihtasari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu. Na kujifunza kutoka kwenye usanifu mwema wa kifasihi wa Luka na mtiririko wa mawazo.

More

Tungependa kuwashukuru BibleProject na YouVersion kwa kutupa somo hili. Kwa taarifa za ziada, tafadhalo tembelea: www.bibleproject.com na www.youversion.com