Soma Biblia Kila Siku 12/2020Mfano
"Abramu" ni jina alilokuwa nalo kwanza Ibrahimu. Amezaliwa katika ukoo wa Shemu, mwana wa Nuhu. Majina ya ukoo huu yameorodheshwa kuanzia m.10 hadi m.26. Baba yake Abramu ni Tera. Tera aliamua kuhama na familia yake: Wakatoka wote katika Uru wa Wakaldayo, waende nchi ya Kanaani, wakafika mpaka Harani wakakaa huko(m.31). Tera alikusudia kufika "nchi ya Kanaani", lakini hakufika. Safari yake ikakoma Harani, labda kutokana na uzee (m.32, Siku za Tera zilikuwa miaka mia mbili na mitano; Tera akafa katika Harani). Kama una ramani za Biblia, angalia safari yake!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 12/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wathesalonike, Mathayo na Mwanzo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz