Soma Biblia Kila Siku 12/2020Mfano
Nuhu akamjengea BWANA madhabahu; akatwaa katika kila mnyama aliye safi, ... akavitoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu(m.20). Nuhu alimwabudu Mungu! Tunapobatizwa twatiliwa alama ya msalaba, maana twabatizwa katika mautiya Yesu Kristo ili tuondolewe dhambi zetu kwa damu yake (Rum 6:3, Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake?). Nuhu na familia yake waliokoka kutoka katika gharika ya maji. Wokovu huu nao ulitiwa alama ya "msalaba", yaani, vifo vya wanyama; na Bwana akasikia harufu ya kumridhisha(m.21)! Kwa maana, ikiwa damu ya mbuzi na mafahali na majivu ya ndama ya ng’ombe waliyonyunyiziwa wenye uchafu hutakasa hata kuusafisha mwili; basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai? (Ebr 9:13-14).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 12/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wathesalonike, Mathayo na Mwanzo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz