Soma Biblia Kila Siku 12/2020Mfano
Basi Bwana akawatawanya kutoka huko waende usoni pa nchi yote; wakaacha kuujenga ule mji (m.8). Kwa nini Mungu aliwapa lugha mbalimbali ili watawanyike? Kwa sababu aliona wanadamu walitaka kuharibika tena. Walikuwa na kiburi. Walitaka kujifanyia jina. Wakaanza kujenga kitu kikubwa ili wao watukuzwe badala ya Mungu (m.4-5, Wakasema, Haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike mbinguni, tujifanyie jina; ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote.Bwana akashuka ili auone mji na mnara waliokuwa wakiujenga wanadamu). Na Bwana alijua wana uwezo mkubwa mno, uwezo unaoonekana tena siku hizi (fikiria k.m. roketi)! Maana leo mataifa na watu wote wameweza kuwasiliana tena (m.6, Bwana akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya)!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 12/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wathesalonike, Mathayo na Mwanzo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz