Soma Biblia Kila Siku 12/2020Mfano
Maisha ya kawaida ya siku zote yataendelea mpaka pale ambapo ghafla Yesu atarudi. Watakatifu watakuwa wanaendelea na utakatifu na kunyakuliwa. Waovu watakuwa wakiendelea katika uovu kama ule wakati wa Nuhu kabla ya gharika (Mwa 6:5-7, Bwana akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu sikuzote.Bwana akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo.Bwana akasema, Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambaacho na ndege wa angani; kwa maana naghairi ya kwamba nimewafanya). Imetupasa kumwamini Yesu Kristo ili Bwana atakaporudi tupate heshima ya kuishi na Mungu milele. Pia inampasa kila mmoja aliyeamini kukesha, ili Bwana Yesu arudipo mara ya pili wote tukutwe tuko tayari kwenda Naye (1 The 5:1-6, Lakini, ndugu, kwa habari ya nyakati na majira, hamna haja niwaandikie.Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku.Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.Bali ninyi, ndugu, hammo gizani, hata siku ile iwapate kama mwivi.Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa nuru, na wana wa mchana; sisi si wa usiku, wala wa giza.Basi tusilale usingizi kama wengine, bali tukeshe, na kuwa na kiasi).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 12/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wathesalonike, Mathayo na Mwanzo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz