Soma Biblia Kila Siku 12/2020Mfano
Mungu anajali tunavyotendeana duniani. Hapa pana picha ya huzuni kwa waliokuwa na fursa za kuwatendea mema wenzao, hasa wale wanyonge katika jamii, lakini wakapuuza kufanya hivyo. Pamoja na picha hii, katika neno la leo lipo neno la ajabu: kwamba hao wasiohesabika kuwa kitu, wako mbele zetu kama Bwana wetu mwenyewe! Kuwapuuza ni sawa na kumpuuza Kristo mwenyewe. Mimi na wewe tunapaswa kuadibishwa na kubidishwa na ujumbe huu. Tuwatendee wenzetu mema kadri tulivyojaliwa. Tutajatoa hesabu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 12/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wathesalonike, Mathayo na Mwanzo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz