Soma Biblia Kila Siku 12/2020Mfano
Neema huenda sambamba na haki ya Mungu. Hiyo huthibitishwa kwa namna mbili, waumini wakiteswa kwa ajili ya Yesu: 1. Mungu ana haki, akiwapa raha na utukufu pamoja na Yesu. Wastahili ufalme wake, si kwa sababu ya kuvumilia kwao, bali kwa sababu saburi yao huthibitisha imani yao kwamba i hai. 2.Mungu ana haki, akiwahukumu wale waliowaudhi, maana tendo hilo huthibitisha uovu wao. Maangamizi yao ni sawa na kutengwa milele na Mungu na baraka na neema yake (m.9,Wataadhibiwa kwa maangamizi ya milele, kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake). Yesu mwenyewe ataitekeleza hukumu hiyo, akija.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 12/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wathesalonike, Mathayo na Mwanzo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz