Soma Biblia Kila Siku 12/2020Mfano
Paulo anaeleza sababu yake kuwaandikia Wathesalonike tena: Wasidanganywe kuamini kwa njia ya maaguzi au barua zisizo halisi kwamba siku ya Bwana Yesu inayokaribia imeshatokea. Maana kabla Yesu hajaja, lazima mambo mawili yatokee: 1.Ule ukengeufu utakaokuwa uasi mkubwa juu ya amri za Mungu na kweli ya Injili. Ukengeufu huu utatokea, wengine kati ya Wakristo watakaporudi nyuma. 2. Yule mtu wa kuasi, yaani mpinga Kristo ambaye maana ya jina lake ni a:kumpinga Kristo, na b:kujiweka mahali pa Kristo, akijidai kuwa Mungu (m.4, Yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 12/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wathesalonike, Mathayo na Mwanzo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz