Soma Biblia Kila Siku 12/2020Mfano
Zamani Mungu alisema nasi kwa njia ya manabii, na hakika walifanya kazi kubwa ya kueneza ujumbe wa Mungu. Kwa sasa Yesu amekuja kwetu, hivyo twaweza kuzungumza naye moja kwa moja. Yesu ameondoa kiambaza kilichotutenga na uwepo wa Mungu alipofanya utatakaso wa dhambo (m.3, akiisha kufanya utakaso wa dhambi). Amekuja kutuletea wokovu. Uwepo wake kwetu ni mng’ao wa wokovu kwetu katika maisha yetu. Hii ni neema ya ajabu. Mwamini Yesu, nawe utapata wokovu na kuwa mrithi wa uzima wa milele.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 12/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wathesalonike, Mathayo na Mwanzo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz