Soma Biblia Kila Siku 12/2020Mfano
Stefano ni mfano hai kwamba siku zote Shetani humchukia mtu anayemtangaza Yesu. Yeyote anayemshuhudia Yesu, hufanyika adui wa Shetani. Lakini ni heri kuwa adui wa Shetani kuliko kuwa adui wa Mungu! Maana Shetani hana jambo lolote jema analomwazia mwanadamu. Shetani humfurahia mtu mwoga, lakini humwogopa mtu aliye jasiri wa Mungu. Basi, tusimwogope Shetani wala mateso. Tusiache kumtangaza Yesu. Pamoja na mateso, tuwe jasiri, na tusiwahesabie dhambi wanaotutesa bali tuwasamehe.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 12/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wathesalonike, Mathayo na Mwanzo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz