Soma Biblia Kila Siku 12/2020Mfano
Wakati huu wa Krismasi, tunakumbuka kuzaliwa kwa Bwana wetu Yesu Kristo hapa duniani. Hii haina maana kuwa huu ni mwanzo wa uwepo wake. Yesu alikuwepo mbinguni, alishiriki kuumba ulimwengu, na baadaye aliamua kufanyika mwili na kuzaliwa kwetu ili kutukomboa. Yeye ni Imanueli, yaani, Mungu pamoja nasi. Ujio wake unatuonyesha upendo wake kwa wanadamu. Basi, tusifanane na wale ambao hawakumpokea, bali tumpende kwa moyo wote. Yesu ni ufunguo wa uzima wa mbinguni. Mwamini, nawe utafanyika mtoto wa Mungu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 12/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wathesalonike, Mathayo na Mwanzo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz