Soma Biblia Kila Siku 12/2020Mfano
Zaburi hii inatukumbusha kuwa BWANA ndiye mwenye fadhili, kila mstari ukifafanua maana yake: Ndiye Mungu mwema na wa pekee aliye wa kweli. Ana hekima kamili, naye aliumba vitu vyote. Tena ni Mwokozi aliwaokoa Waisraeli kutoka utumwa wa Misri na kuwaweka huru. Ndiye Mungu wetu pia. Kuokolewa kwetu kutoka utumwa wa dhambi na kuwekwa huru ni tendo lake kuu. Ni wajibu wetu kudumu katika kumshukuru kwa neema hii tusiyoistahili. Ndipo maisha yetu yatakuwa na amani na baraka za Mungu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 12/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wathesalonike, Mathayo na Mwanzo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz