Soma Biblia Kila Siku 12/2020Mfano
Kabla Yesu hajaja, waumini huhitaji faraja na maonyo (2:13-3:15) juu ya kusimama imara katika imani. Hiyo yawezekana tu tunapolishika Neno la Mungu, tukikubali kuipenda ile kweli. Maana kwa njia hiyo Mungu hutuita tuwe watu wake (m.14, Aliwaitia ninyi kwa injili), kututakasa (m.13, kutakaswa na Roho, na kuiamini kweli; taz. pia Yn 17:17, Baba, uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli), kutupa tumaini jema, na kutufariji (m.16-17, Akatupa faraja ya milele na tumaini jema, katika neema, awafariji mioyo yenu). Hivi tutaimarika wenyewe kiimani, na maisha yetu yote ya kila siku yatashuhudia neema na wema wake Mungu (m.17, kuwafanya imara katika kila neno na tendo jema). Angalia pia aya hizi zinavyomshuhudia Paulo. Ndiye mfano mzuri wa neno katika 1 The 5:17, Ombeni bila kukoma.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 12/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wathesalonike, Mathayo na Mwanzo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz