Soma Biblia Kila Siku 12/2020Mfano
M.11 unaanza na “kwa hiyo”, kwa sababu maombezi ya Paulo yatokana na alivyoandika katika 1:5 kwamba Wathesalonike wastahili Ufalme wa Mungu. Mungu aliyewaita wawe watoto wake, mwenyewe atawastahilisha pia, akiwajaza nia ya kutenda mema. Maana yake si kwamba kazi yao itawastahilisha, maana ni kazi ya imani(m.11, kila kazi ya imani), yaani waokolewa kwa neema (m.12, Jina la Bwana wetu Yesu litukuzwe ndani yenu, nanyi ndani yake, kwa neemaya Mungu wetu). Angalia kwamba imani hutuunganisha na Yesu namna hii kwamba yeyeanatukuzwa, imani yetu katika yeye ikitenda kazi ndani yetu, na sisitutatukuzwa, Yesu akija kwa utukufu (m.12; ling. Kol 3:4, Kristo atakapofunuliwa, aliye uhai wetu, ndipo na ninyi mtafunuliwa pamoja naye katika utukufu).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 12/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wathesalonike, Mathayo na Mwanzo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz