Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 11/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 11/2020

SIKU 9 YA 30

Hapa twapewa mafundisho mawili: 1.Kristo alipata mateso, kwa hiyo sisi wafuasi wake tusishangae nasi tukipata mateso, bali tujivike silaha ya nia ile ilealiyokuwa nayo akiteswa Kristo (m.1a). Mateso wanayopata Wakristo ni kwa mfano matukano (m.4). Maana kama tuliwahi kushiriki na wasio Wakristo katika maisha ya dhambi, wanataka turudi kwao na kuwa kama wao tena, Petro anatukumbusha hapo katika m.4. Tafakari pia 1 Pet 2:21: Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake.Na katika Yn 15:18-21 Yesu mwenyewe anasema, Iwapo ulimwengu ukiwachukia, mwajua ya kuwa umenichukia mimi kabla ya kuwachukia ninyi. Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio wake; lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi naliwachagua katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia. Likumbukeni lile neno nililowaambia, Mtumwa si mkubwa kuliko bwana wake. Ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi; ikiwa walilishika neno langu watalishika na lenu.Lakini haya yote watawatenda kwa ajili ya jina langu, kwa kuwa hawamjui yeye aliyenipeleka.2.Tumekwisha achana na dhambi, maana Kristo aliteswa badala yetu kwa ajili ya dhambi zetu. Kumbuka Petro alivyokwisha kuandika katika 2:24, Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti.Na tena katika 3:18, Kristo ... aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu. Dhambi zetu zilichukuliwa na Yesu msalabani, kwa hiyo hazina haki wala nguvu ya kututawala tena!

siku 8siku 10

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 11/2020

Soma Biblia Kila Siku 11/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Mwanzo na 1 Petro. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz