Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 11/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 11/2020

SIKU 11 YA 30

Petro huwatia moyo Wakristo wenye taabu. Kwanza anarudia kusema kwamba wasishangae, maana Kristo naye aliteswa (m.12:Wapenzi, msione kuwa ni ajabu ule msiba ulio kati yenu, unaowapata kama moto ili kuwajaribu, kana kwamba ni kitu kigeni kiwapatacho). Pili anawaambia jambo la ajabu kwamba wafurahi, maana wako heriwakilaumiwa au wakiteswa kwa ajili ya jina la Yesu! (m.13-16: Kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini...Mkilaumiwa kwa ajili ya jina la Kristo ni heri yenu; kwa kuwa Roho wa utukufu na wa Mungu anawakalia.Maana mtu wa kwenu asiteswe kama mwuaji, au mwivi, au mtenda mabaya, au kama mtu ajishughulishaye na mambo ya watu wengine.Lakini ikiwa kwa sababu ni Mkristo asione haya, bali amtukuze Mungu katika jina hilo! Ukipenda kusoma zaidi juu ya jambo hili, angalia maneno ya Yesu katika Lk 6:22-23, na ya mitume katika Mdo 5:40-42). Wako heri kwa sababu: 1.Ni dalili kuwa Yesu kweli yuko ndani yao. 2. Roho wa Mungu huwatia nguvu na ujasiri (m.14). 3.Wana thawabu kubwa Mbinguni!

siku 10siku 12

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 11/2020

Soma Biblia Kila Siku 11/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Mwanzo na 1 Petro. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz