Soma Biblia Kila Siku 11/2020Mfano
Kwa kifo cha Yesu tumekwisha okolewa na dhambi, kwa hiyo tufuate mapenzi ya Mungu (m.2: Tangu sasa msiendelee kuishi katika tamaa za wanadamu, bali katika mapenzi ya Mungu). Katika somo la leo tunafafanuliwa zaidi maana ya kuishi katika mapenzi ya Mungu. Tukeshekatika sala (m.7)! Tupendanekwa juhudi nyingi! Tukifanya hivyo hatuwezi kusengenyana, bali tutasameheana (m.8). Tukaribishanesisi kwa sisi kwa furaha, yaani tuwe na ukarimu (m.9). Kila Mkristo ameipokea karamayake. Isimfanye ajivune bali aitumie kwa kuwahudumia wengine(m.10). Na shabaha kuu ni Mungu atukuzwekatika yote kwa Yesu Kristo (m.11)!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 11/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Mwanzo na 1 Petro. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz