Soma Biblia Kila Siku 11/2020Mfano
Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake; huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu(m.6-7; angalia kwa makini maneno yaliyotiliwa mkazo). Neno hili ni agizokwako unayetaka kujitafutia mwenyewe utatuzi wa mambo yako. Na ni farajakwako uliyekwama katika hali ngumu ya maisha yako. Mungu ni BABA yako! Yeye ni mwepesi sana kutoa kuliko wewe kuomba! Tena hashindwi uwezo wa kukusaidia! Maelezo ya majina mawili: Silvanoalikuwa ni karani wa Petro. Babelini jina la mfano kuhusu mji wa Rumi.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 11/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Mwanzo na 1 Petro. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz