Soma Biblia Kila Siku 11/2020Mfano
Mungu ndiye Mfalme aliyealika, na anaendelea kualika watu waingie katika furaha ya Ufalme wake. Anatumia watumishi mbalimbali kualika. Kati ya waalikwa wengi wanaukataa mwaliko, na Mungu atawaacha katika upotevu wao. Lakini ataendelea kualika wengine, wema kwa wabaya. Hata hivyo ni muhimu kutambua kuwa atakayeamua kuingia hiyo furaha, ni lazima akubali kuvikwa vazi la wokovu, ambalo ni imani katika Kristo. Twaitwa tujikabidhi kwa Yesu atutakase na kutuvika vazi la arusi (Isa 61:10, Nitafurahi sana katika Bwana, nafsi yangu itashangilia katika Mungu wangu; maana amenivika mavazi ya wokovu, amenifunika vazi la haki, kama bwana arusi ajipambavyo kwa kilemba cha maua, na kama bibi arusi ajipambavyo kwa vyombo vya dhahabu).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 11/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Mwanzo na 1 Petro. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz