Soma Biblia Kila Siku 11/2020Mfano

Jana tuliona makundi mawili wakimjaribu Yesu kwa nyakati tofauti. Leo wanaungana ili kupata nguvu zaidi. Lakini Yesu anatumia hali hiyo tena kuwafundisha kuwa imewapasa kumpenda Mungu na wanadamu. Namna gani tunaweza kumpenda Mungu na jirani zetu? Zingatia iliyoandikwa katika m.37-40: Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza.Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako.Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii. Kisha Yesu anawaonyesha kuwa yeye ni Mwana wa Mungu; ndiye aliyetabiriwa katika unabii. Kwa hiyo walipaswa wamwamini badala ya kumchukia. Yesu Kristo yu umoja na Baba, yaani yu Mungu. Kumpinga na kumchukia ni kumkataa Mungu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 11/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Mwanzo na 1 Petro. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz
Mipangilio yanayo husiana

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021

Upendo Wa Bure

Soma Biblia Kila Siku Januari 2021

Soma Biblia Kila Siku Machi 2021

Roho Mtakatifu - Tuna Uwezo Wa Kuwaka Moto Au La?

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo
