Soma Biblia Kila Siku 11/2020Mfano
Kuna uwezekano mkubwa kwamba wana wa Mungu(m.2 na 4) ni malaika wa Mungu walioanguka pamoja na Shetani (ukipenda, unaweza kusoma 2 Pet 2:4-5, Yud 1:6.9 na Ayu 1:6-7 kwa maelezo zaidi). Roho yangu(m.3), maana yake siyoRoho wa Mungu, bali ni ile pumzi ya uhai aliyowapa wanadamu (Mwa 2:7, Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai).Basi siku zake zitakuwa miaka 120(m.3), habari hii ina maana kwamba, kuanzia hapo anapoongea Mungu mpaka wanadamu watakapoangamizwa na gharika, itapita miaka 120. Nuhu peke yake akapata neema pamoja na familia yake, maana alimwamini BWANA (m.8). Katika Ebr 11:7 imeandikwa, Kwa imani Nuhu akiisha kuonywa na Mungu katika habari za mambo yasiyoonekana bado, kwa jinsi alivyomcha Mungu, aliunda safina, apate kuokoa nyumba yake. Na hivyo akauhukumu makosa ulimwengu, akawa mrithi wa haki ipatikanayo kwa imani.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 11/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Mwanzo na 1 Petro. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz