Soma Biblia Kila Siku 11/2020Mfano
Nuhu alijenga safina na kuandaa kila kitu kama Mungu alivyomwamuru (m.5: Nuhu akafanya kama vile Bwana alivyomwamuru.Na m.16, Walioingia, waliingia mume na mke, wa kila kitu chenye mwili, kama vile alivyomwamuru Mungu; Bwana akamfungia [Nuhu]). Angalia kwamba wote walipokuwa wameingia ndani kama Mungu alivyopanga, ndipo BWANAakamfungia. Mwenye kuhukumu ni Mungu. Mungu mwenyewe alifunga mlango wa safina. Na Mungu akishafunga, hakuna mtu anayeweza kufungua. Huenda walikuwepo waliojuta walipoona gharika, lakini walishachelewa! Yesu atakapokuja mara ya pili, itakuwa vilevile. SAFINA ni YESU! Je, umeshaingia? Endelea kuzingatia swali hili, ukisoma Mt 24:36-41 na 25:10-13.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 11/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Mwanzo na 1 Petro. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz