Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 11/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 11/2020

SIKU 26 YA 30

Ndivyo alivyofanya Nuhu, sawasawa na vyote alivyomwamuru Mungu(m.22). Kwa Nuhu twajifunza mambo mawili muhimu: 1.Mungu hufunua kusudi la moyo wake na mipango yake kwa wale wampendao, wala si kwa wengine (kuhusu Nuhu imeandikwa katika m.9 kwamba alikuwa mtu wa haki, mkamilifu katika vizazi vyake; Nuhu alikwenda pamoja na Mungu)! Kwa maana wampendao Mungu ndio wenye masikio na macho ya kiroho. 2.Mtu wa Mungu anaweza kuitwa na Mungu kufanya jambo la ajabu sana ambalo ni ujinga machoni pa watu wasiomwamini Mungu. Kwa mfano, Nuhu alijenga safina (meli kubwa) kwenye nchi kavu. Nasi tuige utii wake! Leo pia zingatia Ebr 11:7, Kwa imani Nuhu akiisha kuonywa na Mungu katika habari za mambo yasiyoonekana bado, kwa jinsi alivyomcha Mungu, aliunda safina, apate kuokoa nyumba yake. Na hivyo akauhukumu makosa ulimwengu, akawa mrithi wa haki ipatikanayo kwa imani.

siku 25siku 27

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 11/2020

Soma Biblia Kila Siku 11/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Mwanzo na 1 Petro. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz