Soma Biblia Kila Siku 11/2020Mfano
Huu ni mfano wa Mungu alivyojichagulia Israeli wawe watu wake. Lakini hawakuwa waaminifu kwake. Ndipo akawaletea manabii wawaonye. Hawakuwakubali. Hatimaye Mungu aliwapelekea Mwanawe Yesu, naye wakamwona kikwazo kwao, wakamwua. Je, sasa Mungu anataka nini? Anataka mimi na wewe tuwe watu wa upande wake hapa duniani. Ni kwa namna gani tutafanyika watu wa upande wa Mungu? Kwa kumwamini Yesu Kristo. Leo, mimi na wewe tunaitwa tumwamini Yesu ili tufanyike taifa jipya la Mungu!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 11/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Mwanzo na 1 Petro. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz