Soma Biblia Kila Siku 11/2020Mfano
Mtume Petro hachoki kusema juu ya wokovu ulio katika Yesu Kristo. Sisi wahubiri wa Injili tufuate mfano wake katika huduma yetu ili watu wamwone Yesuna kumwabudu na kumpenda! Ubatizo unatuokoa, kwa sababu unatuingiza katika safina ambayo ni Yesu (m.21: Mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unaowaokoa ninyi pia siku hizi). Ukiwa ndani ya Yesu yote yaliyotendeka kwake ni yako! Yaani, kuteswa kwake na kufa kwake (m.18), kufufuka kwake (m.21) na kumiliki kwake (m.22), yote ni yako. Maana alifanya yote kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu (m.18)! Yesu alithibitisha hiyo katika Mk 16:16 akisema, Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 11/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Mwanzo na 1 Petro. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz