Soma Biblia Kila Siku 11/2020Mfano
Ukristo wetu unatakiwa uonekane hasa siku za shida na taabu. Hapo ndipo itaonekana hasa kuwa kuna roho gani ndani yako, na kimbilio lako ni nani! Maana huu ndio wema hasa, mtu akivumilia huzuni kwa kumkumbuka Mungu, pale ateswapo isivyo haki(m.19). Kuwa na roho ya jinsi hiyo ni kuwa na Roho wa Kristo ndani yetu, maana ndivyo alivyokuwa yeye: Alipoteswa, hakuogofya; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki(m.23). Je, umekuwa na tabia gani mbele ya mwajiri wako? – Ukiwa na nafasi tafakari pia Rum 12:17-21, Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote. Kama yamkini, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote.Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana.Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake.Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 11/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Mwanzo na 1 Petro. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz