Soma Biblia Kila Siku 09/2020Mfano
Tukumbushana kwanza maneno ya Yesu katika Mt 5:13-16, Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee? Haifai tena kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu. Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima.Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani.Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni. Moja ya mambo makuu yaliyochangia kuboresha huduma ya Injili wakati wa mtume Paulo na wenzake ni kuwepo kwa uwazi, ukweli na uwajibikaji. Haya yaliwezekana kwa vile mitume hawa walijitoa kwanza kwa Yesu Kristo. Kwa hiyo, walizuia mianya yote yenye kusababisha wengine kujikwaa. Fedha na matumizi yake kanisani na kwingineko ni kiwazo kikubwa cha kukua na kupanuka kwa Injili. Wakristo walitoa, kwa hiyo pia washiriki katika kujua mapato na matumizi ya sadaka ile. Rudia m.20-21, Tukijiepusha na neno hili, mtu asije akatulaumu kwa habari ya karama hii tunayoitumikia; tukitangulia kufikiri yaliyo mema, si mbele za Bwana tu, ila na mbele ya wanadamu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 09/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wakorintho na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Nos gustaría agradecer a Soma Biblia por brindar este plan. Para mayor información por favor visite: http://www.somabiblia.or.tz