Soma Biblia Kila Siku 09/2020Mfano
Utawala wa Mungu unakua na kuenea kwa njia ya kuhusika kwa Wakristo katika kujitoa katika kusaidia wengine. Huduma hii ya utoaji ilifanya kazi ya kuokoa maisha ya jamii maskini kule Yerusalemu. Jambo linalokuza utoaji wa nafsi, mali, wakati na maisha ni jinsi Kristo mwenyewe alivyojitoa kwanza. Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele (Yn 3:16). Yesu Kristo ndiye mfano mkuu wa kujitoa kwetu katika kusaidia na kuokoa. Kipimo kikuu ni Mwokozi wetu. Ukitaka kuangalia zaidi jambo hili, utafute kusoma Lk 19:1-10, Mdo 2:41-47 na 4:32-36.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 09/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wakorintho na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Nos gustaría agradecer a Soma Biblia por brindar este plan. Para mayor información por favor visite: http://www.somabiblia.or.tz