Soma Biblia Kila Siku 09/2020Mfano
Ezekieli alishtushwa sana alipoambiwa na Mungu kuwa “tunu” yake, yaani, mke wake atakufa, lakini yeye Ezekieli asioneshe dalili yoyote ya kuhuzunika (m.15-18). Hii ilimaanisha kuwa wakati hekalu litakapopigwa, mioyo ya Waisraeli waliokuwa utumwani itawauma, lakini hawataweza kuomboleza kwa wazi (m.22-23,Mtafanya kama mimi nilivyofanya; hamtaifunika midomo yenu, wala kula chakula cha watu.Na vilemba vyenu vitakuwa juu ya vichwa vyenu, na viatu vyenu miguuni mwenu; hamtaomboleza wala kulia; lakini mtafifia katika maovu yenu, na kuugua kila mtu pamoja na mwenziwe). Hebu tujadiliane swali hili: Unajisikiaje unapokuwa umeonywa jambo fulani ukalipuuza halafu unashuhudia uharibifu ambao wewe umeusababisha kwa kutotimiza wajibu wako?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 09/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wakorintho na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Nos gustaría agradecer a Soma Biblia por brindar este plan. Para mayor información por favor visite: http://www.somabiblia.or.tz