Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 06/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 06/2020

SIKU 4 YA 30

Kujitakasa kama Yesu alivyo mtakatifu (m.3: Kila mwenye matumaini haya katika yeye [Yesu]hujitakasa, kama yeye alivyo mtakatifu), kinyume chake ni kuishi katika dhambi, yaani, kukaa na dhambi katika maisha yetu. Ni kufanya uasi. Maisha katika dhambi hayapatani na kukaa katika Yesu (m.5-6: Yeye alidhihirishwa, ili aziondoe dhambi; na dhambi haimo ndani yake. Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi; kila atendaye dhambi hakumwona yeye, wala hakumtambua), kwa sababu anataka kutuokoa katika maisha hayo na kututenga na dhambi zetu, na pia Yeye mwenyewe hakutenda dhambi. Ujumbe wa hapa kwamba Mkristo wa kweli hatendi dhambi si kinyume cha habari alizoziandika Mtume katika 1:8 na 10: Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu. … Tukisema kwamba hatukutenda dhambi, twamfanya Yeye kuwa mwongo wala neno lake halimo mwetu. Katika mlango huu wa 3 inafafanuliwa hali ni kukaana dhambi - kuishikatika dhambi. Mfano wa usemi mbovu wa wanaoishi katika hali hiyo: ‘Hayo siyo shida, kwa kuwa Mungu ni upendo, atanisamehe tu!’ Rudia m.8-9: Atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi. Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu. - Tusijidanganye!

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 06/2020

Soma Biblia Kila Siku 06/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Yohana, Ayubu na Mathayo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz