Soma Biblia Kila Siku 06/2020Mfano
Wapenzi, ikiwa Mungu alitupenda sisi hivi, imetupasa na sisi kupendana (m.11). Mungu hukaa ndani yetu, na pendo lake limekamilika ndani yetu (m.12). Hayo yanatuambia kuwa imetupasa tupendane. Lakini kuna zaidi, kwani kuna utajiri ndani yake. Yaani, tukiambatana naye, hutubeba na kutuongoza. Tumeunganishwa na Yohana, kama anavyoandika tena na tena, kwa mfano katika m.14,Sisi tumeona na kushuhudia ya kuwa Baba amemtuma Mwana kuwa Mwokozi wa ulimwengu. Kwa kutumia neno hili “sisi”, pia tunakumbushwa kuwa kumwamini Yesu ni kuamini kuwa Mungu alitupenda, na ni kumfahamu Mungu kama alivyo. Mungu ni upendo. Tujiangalie ili tusikose kupendana sisi kwa sisi tulio watoto wake.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 06/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Yohana, Ayubu na Mathayo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz