Soma Biblia Kila Siku 06/2020Mfano

Hilo ndilo pendo (m.10). Yesu Kristo alileta upendo. Tupendane sisi kwa sisi kwa kuwa pendo lilifunuliwa katika Yesu Kristo ambaye Mungu alimtuma duniani kwa ajili yetu ili kutufanyia upatanisho unaotuletea kuishi na Mungu. Anayempenda ndugu yake katika Kristo amezaliwa na Mungu (rudia 3:14 na 2:3 tunaposoma: Sisi tunajua ya kuwa tumepita toka mautini kuingia uzimani, kwa maana twawapenda ndugu. Yeye asiyependa, akaa katika mauti. … Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye, ikiwa tunashika amri zake). Tupate uzima kwa yeye (m.9). Upendo wa Mungu huonekana katika mioyo yetu, tukimwona Yesu, aliyetumwa na Mungu si kwa ajili ya kutuhukumu bali tupate uzima. Kumbuka ilivyoandikwa katika Yn 3:16-17: Jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Je, umepata nafasi kumwona Yesu katika maisha yako?
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 06/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Yohana, Ayubu na Mathayo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz