Soma Biblia Kila Siku 06/2020Mfano
Msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho (m.1). Kuna sauti nyingi kati yetu. Je, tufanye nini ili tuzitambue hizo roho? Tunapata jibu lenyewe katika m.2: Mwamjua Roho wa Mungu, kila roho ikiriyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokana na Mungu. Ukweli umo katika Yesu Kristo. Zingatia ilivyoandikwa katika Yn 1:14: Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli. Katika ukiri wa Yesu Kristo itatambulikana ikiwa mtu ana roho kutoka kwa Mungu au kutoka kwa mpinga Kristo, Shetani. Watu wenye roho ya mpinga Kristo husema kama dunia inavyotaka kusikia kwa kutumia mawazo ya dunia hii. Hawa wanaacha Neno la Mungu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 06/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Yohana, Ayubu na Mathayo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz