Kusikia Kutoka Kwa Mungu Kila AsubuhiMfano
![Kusikia Kutoka Kwa Mungu Kila Asubuhi](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F19381%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Makao ya Roho wa Mungu
Kristo akae mioyoni mwenu kwa imani mkiwa na shina na msingi katika upendo (WAEFESO 3:17)
Iwapo umeokoka, kwa matumaini unajua kuwa Yesu anaishi ndani yako kupitia kwa nguvu za Roho Mtakatifu. Swali ni, Mungu ana utulivu ndani yako? Anahisi yuko nyumbani ndani yako? Hata ingawa Roho wa Mungu anaishi ndani yako, vitu vingine vinaishi ndani yako pia- kama vile woga, hasira, wivu, au kunung’unika na kulalamika.
Wakati mmoja Mungu alinipa mfano wa jinsi ilivyo kwake Yeye kuishi katika moyo uliyo na manung’uniko, malalamiko, na kutoelewana. Je, ukienda katika nyumba rafiki yako na rafiki yako aseme, “Oh, ingia ndani. Nitakupa kikombe cha kahawa. Jitulize hapo na ujihisi uko nyumbani.” Halafu rafiki yako aanze kumpigia mumewe kelele na hao wawili warushiane maneno na kusemeshana kama wendawazimu mbele yako. Utakuwaje na utulivu katika hali kama hiyo ya kutoelewana?
Ukitaka kuwa makao ya utulivu ya Roho wa Mungu, lazima tuachane na vitu ambavyo hutusababisha kusahau uwepo wake au vinavyomkasirisha. Lazima tukome kunung’unika, kuruhusu utesi na kutotulia ndani yetu au kutokusamehe. Badala yake tunafaa kuhakikisha kuwa maisha yetu ya ndani yanahushughulika na vitu vinavyompendeza na kutukuza uwepo wa Mungu. Midomo yetu ijae sifa na shukrani. Tunafaa kuamka kila siku na kusema mioyoni mwetu, “Habari za asubuhi Bwana, nataka ujihisi kuwa uko nyumbani na utulie ndani yangu leo.”
Sisi wote tunahitaji kuchukua hesabu ya mambo yanayofanyika katika mioyo yetu kwa sababu ni makao ya Mungu. Tunachunguza maisha yetu ya ndani, tunatazama mahali patakatifu ambapo Mungu amechagua kufanya makao yake. Acha tujitolee kumstarehesha ndani yetu.
NENO LA MUNGU KWAKO LEO
Hakikisha kwamba wewe ni makao matulivu kwa Roho wa Bwana.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
![Kusikia Kutoka Kwa Mungu Kila Asubuhi](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F19381%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Ibada hii inatoa mawaidha mafupi, yenye kuwezesha ambayo yatakuhimiza na kukusaidia kupanga wakati na Mungu kipaumbele chako cha juu, kukuza hamu ya muda wa kila siku naye, kuelewa majibu yake kwa maombi yako, na kudumisha uhusiano wako huku ukitumia wakati wa kibinafsi zaidi na Mungu. Anza siku yako na mtu ambaye hakupendi tu bali pia ana majibu yote ambayo utawahi kuhitaji!
More
Tunapenda kuwashukuru Joyce Meyer Mawaziri kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tv.joycemeyer.org/kiswahili/
Mipangilio yanayo husiana
![Ibada juu ya Vita vya Akilini](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F21337%2F320x180.jpg&w=640&q=75)
Ibada juu ya Vita vya Akilini
![Kuwa Karibu Na Mungu Kila Siku](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F26551%2F320x180.jpg&w=640&q=75)
Kuwa Karibu Na Mungu Kila Siku
![Soma Biblia Kila Siku 11/2020](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F22531%2F320x180.jpg&w=640&q=75)
Soma Biblia Kila Siku 11/2020
![Upendo Wa Bure](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F26579%2F320x180.jpg&w=640&q=75)
Upendo Wa Bure
![Moyo - Neno La Mungu Hugeuza Moyo](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F22660%2F320x180.jpg&w=640&q=75)
Moyo - Neno La Mungu Hugeuza Moyo
![Roho Mtakatifu - Tuna Uwezo Wa Kuwaka Moto Au La?](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F26578%2F320x180.jpg&w=640&q=75)
Roho Mtakatifu - Tuna Uwezo Wa Kuwaka Moto Au La?
![Soma Biblia Kila Siku Machi 2021](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F24503%2F320x180.jpg&w=640&q=75)
Soma Biblia Kila Siku Machi 2021
![MWANGA Kuvutiwa Maishani Na Mwanga Ajabu Wa Mungu](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F21139%2F320x180.jpg&w=640&q=75)
MWANGA Kuvutiwa Maishani Na Mwanga Ajabu Wa Mungu
![Soma Biblia Kila Siku Julai 2021](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F26577%2F320x180.jpg&w=640&q=75)
Soma Biblia Kila Siku Julai 2021
![Soma Biblia Kila Siku 07/2020](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F20586%2F320x180.jpg&w=640&q=75)