Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kusikia Kutoka Kwa Mungu Kila AsubuhiMfano

Kusikia Kutoka Kwa Mungu  Kila Asubuhi

SIKU 2 YA 14

Usaidizi Uko Hapa

Nami nitamwomba Baba, naye atawapa msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele, ndiye Roho wa kweli (Mshauri, Msaidizi, Mwombezi, Mtetezi, Mtiaji nguvu, na Mlinzi) akae nanyi milele. (YOHANA 14:16)

Watu wengi wamempokea Yesu kama mwokozi na Bwana. Wataenda mbinguni, lakini hawafuarahii uwezo wa Roho Mtakatifu unaopatikana kwa ukamilifu wote au kufurahia ushindi wa kweli ambao Mungu anataka wafurahie duniani. Kurahisisha mambo, wengi wanakwenda mbinguni lakini hawaifurahii safari.

Mara nyingi, tunawatazama wale walio na mali, vyeo, uwezo, umaarufu na rasilimali nyinginezo kwa wingi na tunawachukulia kuwa “wamefanikiwa.” Lakini watu wengi wanaodhaniwa kuwa wana mafanikio bado wanakosa uhusiano mwema, afya njema, amani, furaha, kuridhika, na baraka zingine za kweli kupitia kwa uhusiano wa kibinafsi na Yesu Kristo. Watu kama hao bado wanajitegemea; hawajajifunza kutegemea nguvu za Roho Mtakatifu kikamilifu.

Watu wanaojitosheleza wenyewe binafsi mara nyingi hufikiri kwamba kumtegemea Mungu ni ishara ya udhaifu. Lakini ukweli ni kwamba, kwa kutumia nguvu za Roho Mtakatifu, wanaweza kutekeleza mengi zaidi kuliko kama wanafanya kazi kwa nguvu zao wenyewe.

Mungu alituumba kwa njia kwamba, ingawa tuna nguvu, tunao pia udhaifu na tunahitaji msaada wake. Tunajua kwamba anataka kutusaidia kwa sababu alituma Masidizi wa kiungu, Roho Mtakatifu kuishi ndani yetu (soma 1 Wakorintho 6:19).

Tunang’ang’ana bila sababu kwa sababu hatupokei usaidizi uliopo kwa ajili yetu. Ninakuhimiza kumtegemea, sio kwa nguvu zako. Chochote unachokabiliana nacho, si lazima ukabiliane nacho peke yako. 

NENO LA MUNGU KWAKO LEO

Siku yako mbaya sana na Mungu itakuwa nzuri zaidi ya siku yako nzuri kabisa bila Mungu. Roho Mtakatifu yuko hapa kuzungumza nawe na kukusaidia kwa njia yoyote unayohitaji msaada leo.

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Kusikia Kutoka Kwa Mungu  Kila Asubuhi

Ibada hii inatoa mawaidha mafupi, yenye kuwezesha ambayo yatakuhimiza na kukusaidia kupanga wakati na Mungu kipaumbele chako cha juu, kukuza hamu ya muda wa kila siku naye, kuelewa majibu yake kwa maombi yako, na kudumisha uhusiano wako huku ukitumia wakati wa kibinafsi zaidi na Mungu. Anza siku yako na mtu ambaye hakupendi tu bali pia ana majibu yote ambayo utawahi kuhitaji!

More

Tunapenda kuwashukuru Joyce Meyer Mawaziri kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tv.joycemeyer.org/kiswahili/