Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Uhakika katika siku za mashakaMfano

Certainty In Times Of Uncertainty

SIKU 4 YA 5

Wakati mwingi mambo hayaendi kulingana na mipango yetu lakini yanaambatana na iopango ya Mungu

Maisha pia hayakosi misukosuko njiani. Kushindwa hakupatikani ndani ya misukosuko bali ni wakati tu tunaporuhusu misukosuko kutuzuia safarini.
Usishushwe moyo wakati mambo yanakawia hadi ukose kufuata kusudi lako.Hatuwezi kuzuia mambo yanapokuja kwetu lakini twaweza chagua jinsi ya kushughulikia mambo hayo. Pastor Charles R.Swindoll wakati mmoja alisema kwamba maisha ni asili mia kumi ya yale yanayotutendekea na asilimia tisini na jinsi tunavyoshughulikia mambo hayo.

Wazo lako ni chombo muhimu. Ninaamini kwamba watu ambao wamefaulu hawajafaulu kwa ajili wana talanta sana au wana ujuzi. Watu hao wamefaulu ni sababu ya mawazo yao hata wakati wanaposhindwa.

Ni lazima tutumainie hatua hiyo hata wakati safari inagonga miamba. Mungu anakutengeneza kwa ajili ya mipango aliyokuumba uishi kwayo.

Mungu hutuweka kwa kile ninachokiita " majira ya kujinyoosha" kuandaa mawazo yetu kwa hatima tunayoielekea.

Kuwa na uhakika wakati wa shaka hakumaanishi kufumbia macho.yanayotendeka miongoni mwetu. Haimaanishi kwamba hautakua na hisia za hofu., sisi ni wanadamu tu. Yamaanisha kwamba sisi kama wafuasi wa Kristu twachagua kuwa na imani katikati ya hofu na mawazo kinyume yanayotuzingira. Yamaanisha kwamba hata tukiwa na hofu mawazoni mwetu Bwana atatutwalia tunachohitaji ili kuendelea.

Wakati wa shaka Bibilia yako ni hakikisho

Mungu ni hakikisho

Yesu ameamua

Tazama. Twaweza kuishi kwenye ulimwengu wenye kipimo lakini twamtumikia Mungu asiye na vipimo
siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Certainty In Times Of Uncertainty

Katikati ya mashaka, Mungu ni wa uhakika! Ungana na David Villa katika mpango wake mpya anapoangalia mashaka na hasi ili kufikia kitu kikubwa.

More

Tunapenda kumshukuru David Villa kwa kutupa mpango huu. Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea: https://davidvilla.me