Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Uhakika katika siku za mashakaMfano

Certainty In Times Of Uncertainty

SIKU 2 YA 5

Katika karne ya kidigitali, taarifa tunazipata haraka sana kuliko zamani.

Unaweza kutafuta kwenye Google chochote unachotaka, na unaweza kusoma juu ya somo hilo wiki kadhaa. Kwa kubofya puku (mouse), au kubofya kwa kidole chako, unaweza kujifunza vyote unavyotaka. Wakati hii hatua chanya kwa wakati tunaoishi, sivyo ilivyo siku zote. Katika wingi wa taarifa kuna wingi pia wa taarifa potofu. Taarifa zinazovuma sana hatuwezi kujua zilizo za kweli au za uongo.

Tofauti kati ya kweli na mawazo imefunikwa na waandishi wa habari na vituo vya habari ambavyo havitafuti ukweli kama mimi na wewe.

Wanatafuta kukadiriwa.

Watu wanapokuwa waoga, wataangalia habari. Wanataka aidha kufarijiwa au kutaarifiwa kuhusu wanachokiogopa. Bado, mara nyingi tunachukua maneno ya mtu kuwa ukweli. Tunasoma na kusikiliza na kudhani kwamba chochote kilichoandikwa au tulichoambiwa ni halisi, pasipo kufikiria kwamba chanzo tunachokitazama kinaweza pia kupotoshwa.

UKWELI pekee tunaojua ni kwamba Yesu Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu. Ukweli pekee tunaoujua umethibitishwa, umenukuliwa, ni kwamba Mungu atakuwepo kuanzia mwanzo mpaka mwisho. Kwa kufungua na kufunga. Yeye ni mwandishi na mhariri, na neno lake ni mwisho. Hakuna kitu cha kupambwa pambwa. Hakuna ukweli ambao Mungu bado hajaufunua.

Sijakuambia uache kusoma habari. Kuacha kuwaamini wale wanaokuzunguka. Ninachokuambia ni kwamba pasipo kujali kilichoandikwa, pasipokujali kilichotaarifiwa, Mungu tayari anajua. Mipango ya Mungu juu yako haibadiriki kwa sababu ya wanadamu. Mipango ya Mungu ni thabiti, na haitegemei yale yanayotuzunguka.

Katika nyakati za mashaka, Mungu ni thabiti. Japo mipango yetu inaweza kushindwa na kubadirika, mipango ambayo Bwana anayo kwa ajili yetu itatuvusha.

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Certainty In Times Of Uncertainty

Katikati ya mashaka, Mungu ni wa uhakika! Ungana na David Villa katika mpango wake mpya anapoangalia mashaka na hasi ili kufikia kitu kikubwa.

More

Tunapenda kumshukuru David Villa kwa kutupa mpango huu. Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea: https://davidvilla.me