Uhakika katika siku za mashakaMfano
Kila siku, watu ulimwenguni pote huwasha Tv na kuangalia habari.
Matukio ya duniani yanajadiliwa karibu kila chaneli.
Hasi ipo kwenye mitandano.
Majarida na magazeti, japo si maarufu kama ilivyokuwa mwanzo, bado yapo mengi.
Hofu na hasi bado vipo kwa wingi, pia.
Huwezi kuzuia. Ipo kwenye nyuso zetu 24/7. Hasi ni janga.
Lakini tunafanya nini?
Tunaongeza sauti.
Tunabofya kiunganishi.
Tunafungua ukurasa unaofuatia.
Na tunaruhusu hasi kuingia akilini mwetu. Tunahofu kuhusu vita inayoendelea, ugonjwa wowote unaosambaa, chochote ambacho kinaendelea katika soko la mitaji.
Kwa nini tunafanya hiki? Ni kitu gani cha kuvutia katika taarifa ya aina hii?
Sisi ni waoga.
Siyo siri kwamba kuna giza nene katika ulimwengu huu, tayari kuwavuta wote walio tayari kusikiliza katika mazingira haya.
Lakini pia kuna mwanga mkubwa.
Na, kuliko na mwanga, giza haliwezi kushinda.
Mwanga ambao siku zote umeniangazia wakati wa siku zangu za giza umekuwa ni neno la Mungu. Kwa sababu pasipo kujali hali unayojikuta, Biblia itakupitisha kila hatua ili kupita. Mgogoro wa kifedha, matatizo kazini, shuleni, majanga ya dunia, vyote vi dhaifu ukilinganisha na Bwana, na umilele. Biblia yako ni chanzo chako cha mwanga usioisha.
Hata katika vyumba vyenye giza nene, wakati taa inapowashwa, mwanga hufukuza giza. Hata katikati ya hali mbaya, katikati ya majanga, katikati ya shida na mashaka, mwanga ambao Bwana anatuangazia bado unashinda. Hakuna mwanga mkubwa zaidi.
Katikati ya giza, nachagua kuukimbilia mwanga. Kuuruhusu kuangazia roho yangu na kuongoza njia kwenye siku zilizo bora.
Kuhusu Mpango huu
Katikati ya mashaka, Mungu ni wa uhakika! Ungana na David Villa katika mpango wake mpya anapoangalia mashaka na hasi ili kufikia kitu kikubwa.
More