Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 04/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 04/2020

SIKU 7 YA 30

Ni vizuri ikiwa watu wa Mungu wanahimizana katika jambo jema, na hasa katika mambo ya ibada (Ebr 10:25,Tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia). Ndivyo somo hili linavyofanya: Watumishi wote wa BWANA wanakumbushwa kumsifu. Kama Wakristo, miili yetu ni hekalu la Mungu (1 Kor 6:19, Hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu). Hivyo 'tumesimama' nyumbani mwake muda wote – hata usiku. Na sote tu watumishi na makuhani wa BWANA (1 Pet 2:5 na 9, Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo. … Ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu). Hivyo kila wakati tunapaswa kumsifu na kumshukuru Mungu wetu aliyetuumba pamoja na vitu vyote. Kristo atatubariki kwa huruma zake.

siku 6siku 8

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 04/2020

Soma Biblia Kila Siku 04/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Luka, Zaburi na Ayubu. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kusoma mpango huu

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz