Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 03/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 03/2020

SIKU 14 YA 31

Daudi alikuwa amepata fundisho. Amejifunza kuwa Mungu ni Mtakatifu. Naye Daudi akamwogopa BWANA siku ile(m.9). Neno la Mungu si mchezo. Lazima lifuatwe sawa sawa. Sasa hawatumii tena gari, bali wanalichukua kwa mikono (m.13). Katika 1 Nya 15:12-15 Daudi anawaambia, Ninyi ni vichwa vya mbari za baba za Walawi; jitakaseni, ninyi na ndugu zenu, ili mlipandishe sanduku la Bwana, Mungu wa Israeli, mpaka mahali pale nilipoliwekea tayari. Kwani kwa sababu ninyi hamkulichukua safari ya kwanza, Bwana, Mungu wetu, alitufurikia, kwa maana hatukumtafuta sawasawa na sheria. Basi makuhani na Walawi wakajitakasa, ili wapate kulipandisha sanduku la Bwana, Mungu wa Israeli. Na wana wa Walawi wakalichukua sanduku la Mungu mabegani mwao kwa miti yake, kama vile Musa alivyoamuru, sawasawa na neno la Bwana. Pia Daudi amejifunza kwamba kweli ni baraka kubwa isiyopimika Bwana akikaa katikati ya watu wake (m.11-12; ukipenda unaweza kulinganisha na 2 Kor 6:16-18 na Ufu 21:1-5). Daudi alimpenda sana Bwana! Furaha ilibubujika moyoni mwake. Lazima acheze! Lakini Mikali alimdharau, kama Yuda Iskariote alivyomdharau Mariamu alipompaka Yesu miguu kwa marhamu ya nardo safi (Yn 12:1-8).

siku 13siku 15

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 03/2020

Soma Biblia Kila Siku 03/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Samweli, Mathayo na Zaburi. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kusoma na mpango huu

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz