Soma Biblia Kila Siku 03/2020Mfano
Mefiboshethi alipofika kwa Daudi akasujudu akisema, Mimi mtumwa wako ni nini, hata ukamwangalia mbwa mfu kama mimi (m.8)? Kawaida ni kwamba mfalme mpya alikuwa anawaangamiza adui zake wote. Kwa hiyo Mefiboshethi alishangaa. Alitambua wazi kuwa hakustahili jambo hili, bali ni neema tu. Mambo mawili yalimsukuma Daudi kufanya hivi: 1. Mwenyewe amepokea neema kubwa kwa Mungu bila kustahili, basi alitaka kuwatendea watu wengine vivyo hivyo (m.3: Mfalme akasema, Je! Hakuna hata sasa mtu ye yote wa nyumba ya Sauli, nipate kumtendea mema ya Mungu?). 2. Agano lake na Yonathani: kwa ajili ya Yonathani (m.1 na 7; habari ya agano kati ya Daudi na Yonathani inapatikana katika 1 Sam 20:12-17).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 03/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Samweli, Mathayo na Zaburi. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kusoma na mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz