Soma Biblia Kila Siku 03/2020Mfano
Katika mlango wa nane tulisoma juu ya vita vya Daudi na Washami (8:3-7). Leo tunasoma tena habari ya vita vile (m.15-19), lakini kwa upana zaidi. Kiini chake ni Washami kuja kuwasaidia wana wa Amoni ambao walikuwa wamemchukiza Daudi kwa tendo baya sana (m.3-4 na 6-7). Tunahitaji kuelewa kuwa Waisraeli walikuwa ni watu wa Bwana, Mungu aliye hai mwenye enzi yote. Kwa hiyo Waisraeli walipokuwa wanaaibishwa na adui ni jina la Bwana lililoaibishwa. Leo Wakristo ni watu wa Mungu. Tukumbuke vita vyetu ni vya kiroho. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho (Efe 6:12). Hivyo silaha yetu ni kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu(1 Pet 2:9-10).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 03/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Samweli, Mathayo na Zaburi. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kusoma na mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz