Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 03/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 03/2020

SIKU 25 YA 31

Mkate huu wa usiku wa Pasaka ni uhalisi wa fumbo la nyama ya kondoo wa Pasaka na mana ya jangwani (unaweza kusoma zaidi katika Kut 12:3-11 na 16:35). Pia ni uhalisia wa fundisho la Yesu katika Yn 6: Mimi ndimi chakula cha uzima; yeye ajaye kwangu hataona njaa kabisa, naye aniaminiye hataona kiu kamwe(m.35). Mimi ndimi chakula cha uzima(m.48). Divai waliyokunywa ni uhalisia wa fumbo la damu iliyowaokoa wana wa Israeli kule Misri. Na sisi kila tulapo mkate na kunywa divai twakiri na kutangaza tumaini la wokovu wetu unaotokana na kazi ya hitimisho ya Yesu Kristo kuutoa mwili na damu yake kwa ukombozi wa wote (ukipenda unaweza kusoma zaidi katika 1 Kor 11:23-33).

siku 24siku 26

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 03/2020

Soma Biblia Kila Siku 03/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Samweli, Mathayo na Zaburi. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kusoma na mpango huu

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz