Soma Biblia Kila Siku 03/2020Mfano
Hapa pana tofauti kati ya Petro na Yuda katika jinsi walivyoishughulikia dhambi. Petro alipotambua dhambi yake, alipondeka, akajuta na kutubu. Bali Yuda alitafuta tu kujihalalisha mwenyewe kwa kutenda aliyofikiri kuwa ni mema, bila kutubu. Kutotubu hufanya dhambi ibaki bila kuondolewa. Madhara ya dhambi yalimpelekea Yuda kujiua. Hii ni athari ya dhambi ya Adamu, baba yetu. Kizazi chake chote kimekuwa chini ya laana ya dhambi ile hata leo. Lakini kuna njia ya kuachana na laana hiyo! Kumbuka kutubu na kumkimbilia Yesu kila utambuapo dhambi.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 03/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Samweli, Mathayo na Zaburi. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kusoma na mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz